Mashindano ya kila mwaka ya KYISA makala ya mwaka huu ambayo ni ya 10 yanayohusisha wachezaji kutoka kaunti mbalimbali mwaka huu yaafanyika katika kaunti ya Homa BAY.
Kulingana na taarifa ni kuwa mashindano hayo yatafanyika katika shule mbalimbali za gatuzi hilo linaloongizwa na Gladys Wanga.
Kati ya shule ambazo zitakuwa wenyeji wa mashindano hayo ni pamoja na shule ya upili ya kinadada ya Asumbi Girls,Pap Kalango, Orero Boys, chuo cha kiufundi cha Asumbi pamoja na shule ya upili ya Wikoteng.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2024 mashindano hayo ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 yalifanyika katika kaunti ya Kilifi katika eneo bunge Malindi.