Naibu msemaji wa serikali kuu Mwanaisha Chidzuga, ametetea mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu nchini, akisema kuwa umesaidia pakubwa wakenya wengi kupata nafasi za ajira.
Chidzuga amesema kuwa zaidi ya vijana laki, mbili wamepata nafasi za ajira kando na akina mama wafanyabiashara, ambao huuza bidhaa za vyakula kwa wale wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini, naibu msemaji huyo wa serikali kuu, amesema kuwa mradi huo kwa sasa, unatekelezwa katika kaunti 36 humu chini.
Aidha, amesema kuwa ili mradi huo ufanikiwe katika kaunti zote 47 za taifa hili, sharti wakenya wauunge mkono kiukamilifu.