Maandamano ya kizazi cha Gen Z, yaliyoshuhudiwa humu nchini mwaka jana 2024, yalichangia pakubwa kwa baadhi ya serikali za kaunti, kushindwa kufanya maendeleo, kama ilivyosema ripoti ya mkaguzi wa bajeti Magaret Nyakang’o .
Kulingama na Naibu gavana wa kaunti ya Lamu, Mbarak Bahjaj serikali ya kitaifa ilichelewa kusambaza fedha kwa serikali za kaunti, ikiwemo ile ya Lamu ambayo iliorodheshwa kutumia asilimia 5 pekee, ya fedha za maendeleo.
Amesema ilikuwa vigumu kupangilia fedha hizo, kutokana na kuwa zilifika kuchelewa jambo ambalo, lilisababisha serikali ya kaunti ya Lamu kutiumia kiasi kidogo cha fedha za maendeleo.
Aidha, amesema kwa sasa miradi mbalimbali imeanzishwa na inaendelea na kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa kifedha, kaunti ya Lamu itakuwa na mabadiliko makubwa katika utumizi wa fedha zake za maendeleo.