Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah anayechezea klabu ya Liverpool kule Uingereza ndiye mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufikisha mabao 20 katika misimu saba mfululizo.
Mo Salah alifikisha mabao ishirini yake msimu huu usiku wa kuamkia leo alipofunga dhidi ya Sparta Prague katika ushindi wa mabao 6-1 uliopeleka Liverpool hatua ya robo fainali kwenye ligi ya Uropa.
Huku hayo yakijiri kuna tetesi za mzozo unaomhusisha mechazaji huyo kwani timu yake ya taifa ya Misri inamhitaji katika mashindano ya kimataifa kwenye pumziko lijalo huku klabu ya Liverpool ikiwa inasema ni mchezaji ambayo bado yupo na jeraha wanamhudumia kwani hajapona kikamilifu licha ya kuwa anachezeshwa katika mechi.

