MKONDONI FC YAANDIBIWA NA FKF

Klabu ya Mkondoni Fc inayocheza ligi ya eneo bunge la Malindi Kaunti ya Kilifi imefungwa kutotumia uwanja wao wa nyumbani hadi mwisho wa msimu huu.

Nahodha wa timu hiyo Chambele pia amepigwa ya kuchezea klabu yoyote ya FKF eneo bunge hilo kwa muda usiojulikana.

Haya yanatokana na vurugu lililosababishwa na mashabiki pamoja na nahodha huyo kumvamia refa kwa kile walichokuwa wanakimtaja kama maonevu katika maamuzi.

Katika mechi hiyo Mkondoni walipoteza kwa 3-1 dhidi ya Real Malindi katika uwanja wa shule ya Msingi ya Mkondoni

Kwa sasa klabu ya Mkondoni italazimika kutumia uwanja wa Maji Bombers Lango Baya au uwanja wa Kakoneni hadi mwisho wa msimu kama adhabu ya vurugu hilo