Kamati ya mashindano ya soka ya fkf nchini imeipa klabu ya kakamega Homeboyz ushindi wa alama tatu na mabao mawili kutokana na vurugu lililosababishwa na AFC Leopards katika mechi ya ligi kuu siku ya jumapili katika uwanja wa bukhungu.
AFC Leopards pia wamepunguziwa alama tatu kama adhabu, mashabiki wa klabu hiyo wamepigwa marufuku ya kutamazama mechi nne mfululizo kwa kusababisha vurugu, pamoja na klabu hiyo kupigwa faini ya shilingi laki tano.
Ingwe pia wamepewa sharti la kusimamia matibabu ya refa wa mechi hiyo Michael Obuya aliye jeruhiwa na mashabiki

