Mwana riadha nguli wa Kenya, Eliud Kipchoge, amesema kwamba kuwepo kwa maumivu katika mguu wake kati kati mwa mbio za Boston Marathon ndio jambo lililomponza na kumaliza nafasi ya sita siku ya Jumatatu.
Katika mbio hizo ambazo Evans Chebet alimshinda na kumaliza nafasi ya kwanza, Kipchoge anasema kwamba katika kilomita ya 30 alianza kuhisi maumivu hivyo akalazimika kupunguza mwendo na kumaliza mbio hizo za kilomita 42 kwa masaa mawili na dakika tisa ambao ni muda mrefu zaidi kwa bingwa huyo wa Olimpiki kuwahi kumaliza katika mbio za dunia.
Hata hivyo Kipchoge amesema kwamba ako na imani kubwa ya kutetea ubingwa wake wa Olimpiki jijini Paris ufaransa mwaka ujao baada ya kukosa mafanikio katika mashindano ya Boston Marathon ambayo alikuwa anashiriki kwa mara ya kwanza

