Mwanariadha kutoka Kenya Evans Chebet jana alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa Boston Marathon katika mashindano yaliyofanyika jana katika taifa la marekani.
Chebet alikamilisha mbio hizo za kilomita 42 kwa masaa 2.05.54 akimshinda mtanzania Gabreal Geay aliyemaliza kwa muda wa masaa 2.06.04.
Bingwa wa Olimpiki mara mbili Eliud Kipchoge ambaye wakenya wengi walikuwa na matarajio makubwa naye jana alimaliza katika nafasi ya 6.
Kwa upande wa kinadada Hellen Obiri aliwakilisha taifa la Kenya vyema kwa kushinda ubingwa wake wa kwanza kabisa katika mbio hizi ndefu za Boston Marathon akimaliza kwa masaa 2.21.38.

