Ukosefu wa sheria madhubuti za kushtaki wapangaji wa matokeo ndio jambo kubwa linalo athiri soka la Kenya kwa sasa.
Ni kauli ya Nick Mwendwa ambaye amerejea madarakani mwa urais wa FKF baada ya kuwepo nje kwa muda akishughulikia kesi za uporaji wa hela za michezo.
Ameyazungumza hayo alipokutana na kamati ya bunge inayosimamia michezo na utamaduni na kusema kwamba kwa sasa kama shirikisho wanalemewa na visa vingi vya upangaji wa matokeo akisema kwamba kwa sasa hakuna sheria maalumu za kuwafunga wanaopatikana na hatia.
Nick Mwendwa amesistiza kwamba bunge linajukumu sasa ya kuunda sheria zitakazofanya washtakiwa kuhukumiwa vilivyo ili kupunguza kuwepo kwa visa kama hivyo.

