Klabu ya Chelsea sasa imeagana rasmi na mashindano ya klabu bingwa ulaya baada ya kukubali kichapo cha raundi ya pili dhidi ya Real Madrid darajani Stamford Bridge usiku wa kuamkia leo.
The Blues wametandikwa mabao 2-0 na mabao ya kinda wa Brazil Rodrigo ndio mabao yaliyotosha kuipeleka Real Madrid ya mkufunzi Carlo Ancelotti katika hatua ya semi fainali.
Kwengine ni kwamba AC Milan wamelazimisha Napoli sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Diego Armando Maradona.
Sare hiyo imewafaa Ac Milan kwani sasa wamefuzu kuingia hatua ya semi fainali kwa utofauti wa mabao bao kwani jumla ya mabao ni 2-1 kutokana na ushindi wa AC Milan 1-0 katika uwanja wa Sansiro kwenye raundi ya kwanza.
Kwenye mechi hiyo Olivier Giroud, straika mkongwe kutoka Ufaransa aliingia kambani huku straika nguli raia wa Nigeria victor osemhen akifungia Napoli bao la kufutia machozi.

