CHAPISHO ZA KUPUNGUZA VURUGU MAGARINI – FKF

Shirikisho la soka la FKF eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi linapendekeza vilabu vya soka vya ligi hiyo kuchapisha maneno ya ‘No Violence’ katika shati za sare zao.

Kulingana na katibu mkuu wa soka la Magarini Emmanuel Kazungu ni kwamba maneno ya chapisho hizo itasaidia kusambaza ujumbe wa kuhamasisha jamii pamoja na vilabu kupunguza vurugu wakati wa mechi.

Haya yanajiri kipindi ambacho kumekuwepo na vurugu mara kadhaa mashinani ikiwemo hii ya punde zaidi ya mechi ya eneo bunge la Malindi ambapo vurugu lilipelekea mechi ya Mkondoni Fc na Real Malindi ilikatishwa.