Nguli wa klabu ya Paris SG pamoja na timu ya taifa ya Argentina Leonel Messi atakuwa anafufua uhasama wake na Cristiano Ronaldo tarehe 19 mwezi huu wa January ambapo Klabu ya PSG imethibitisha kuwa itakuwa inarindima ngoma dhidi ya baadhi ya wachezaji kutoka Al Nassr pamoja na Al Hilal.
Messi alirejea mazoezini wiki jana baada ya kupewa likizo ya majuma mawili baada ya kushinda ubingwa wa dunia mwezi disemba mwaka 2022.
Wakati hayo yakijiri Ronaldo ambaye sasa atakuwa anafikisha umri wa miaka 38 mwezi ujao alisajiliwa na Al Nassr kwa dau la Euro milioni
200 kwa mkataba utakaodumu hado 2025.

