Afisa mkuu wa kudumu katika michezo kaunti ya Kilifi bwana Naftali Owino analenga kuanzisha timu za vijana wasiozidi umri wa miaka 12 katika soka pamoja na mpira wa kikapu kama mkakati moja wapo wa kukuza talanta za vijana kaunti ya Kilifi.
Katika hotuba yake jana kwenye hafla ya Kilta Awards 2022 katika kanisa la Goshen House of Prayer mjini Malindi alisema kwamba sasa ipo haja ya kuinua vipaji vya vijana kutoka umri mdogo ili kuimarisha hali ya michezo miongoni mwa jamii ya pwani.
Alihakikishia wakazi wa Kilifi kwamba serikali ya kaunti hiyo inalenga kufanikisha miradi mingi ya michezo pamoja na kusaidia vijana kujikwamua kutoka janga la umaskini kupitia talanta ambazo zitawapa kipato.

