MASHINDANO YASHULE ZA UPILI YARINDIMA KWALE

Mashindano ya Riadha za muhula wa kwanza katika shule za upili za gatuzi dogo la Matuga Kaunti ya Kwale, yameanza rasmi leo katika shule ya Upili ya Wavulana ya Kwale.

Takribani Shule 21 zinashiriki katika vitengo mbalimbali ikiwemo ,mbio ndefu na fupi ,mpira wa kikapu , Raga, mpira wa magongo ,handiball, kurusha mkuki, kuruka viunzi na Mbio za kupokezana vijiti.

Riadha hizo zitafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo kesho jumamos ya tarehe 11 ndio itakuwa mwisho.