Masaibu ya klabu ya Wazito fc ligini yanazidi kuonekana huku wakiwa hatarini kushuka daraja la ligi kuu ya fkf msimu huu.
Hii ni baada ya jana kutandikwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards katika mtanangwe uliochezwa dimbani Kasarani.
Klabu hiyo imekuwa na msururu wa matokeo mabaya msimu huu kwani imeshinda mechi mbili pekee kati ya mechi 17 mwaka huu wa 2023.
Akizungumza baada ya mechi hiyo mkufunzi mkuu wa klabu ya Wazito FC Charles Odero anasema ujio wa wachezaji wapya ambao bado hawajashikana miguu ndio jambo ambalo wanafanyia kazi kwa sasa ili kuanza kuandikisha matokeo mazuri.
Kwa sasa Wazito fc wanasimama katika nafasi ya 17 wakiwa na alama 10.

