Mashabiki wa klabu ya Young Bulls wanazidi kueleza kutoridhishwa na matokeo mazuri baada ya jana timu yao kupigwa mabao 5-1 dhidi ya Bumbani Stars nyumbani Alaskan.
Katika mechi ya jana mashabiki walianza kuondoka uwanjani mechi ikiendelea wakidai kuwa matokeo mabaya ya timu hiyo hayawavutii
Licha ya matokeo hayo mashabiki wengi walijitokeza jana wakiwemo viongozi wa kisiasa wa kaunti ya Kilifi. Meneja wa Young Bulls amethibitisha kuwa jana Young Bulls ilikusanya zaidi elfu 15k kama kiingilio pekee
Mashabiki wa klabu ya SS Assad kule Kwale wanasbinikiza klabu hiyo kufanya usajili katika dirisha dogo ili kuimarisha kikosi kipindi hiki ambacho timu inaandikisha matokeo mabaya
Taarifa zasema kuwa wikendi hii uhaba wa wachezaji ulionekana Bayana pale wachezaji 11 pekee na mmoja wa akiba ndio walisafiri kwenda Kisumu kuvaana na Vihiga United
Baadhi ya wachezaji waliachana na timu hiyo kutokana na mikataba yao kutoheshimiwa ambao ni pamoja na Feyswal Dzuya ambaye kwa sasa yuko kwao Mjanaheri eneo bunge la Magarini.

