MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gabriel Jesus, anaweza kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha linaloshukiwa kuwa la mshipa wa goti baada ya kugongana na Bruno Fernandes wa Manchester United.
Fowadi huyo wa Kibrazili alilazimika kutolewa nje ya uwanja dakika za mwisho za kipindi cha kwanza katika pambano la Arsenal la Kombe la FA dhidi ya Manchester United Jumapili.
Jeraha hilo ni la goti lake la kushoto na sio la kulia, ambalo alifanyiwa upasuaji mwaka wa 2022.
Jesus alifanyiwa vipimo siku ya Jumatatu, na vipimo zaidi vitafanywa leo ili kubaini ukubwa wa jeraha lake na atakaa nje kwa muda gani.

