Usalama unatarajiwa kuzidi kuimarika katika kijiji cha kiraho, wadi ya mji wa malindi kaunti ya Kilifi baada ya mwakilishi wadi wa eneo hilo Rashid Odhiambo kuingilia kati Ukukarabati wa taa la mulika mwizi lililokuwa limeharibika kwa takriban miaka mitatu.
Akizungumza baada ya kufanikisha ukarabati huo alasiri ya leo Odhiambo amethibitisha kuwa amekuwa akifanya vikao vya kimaendeleo kwa wiki kadhaa sasa tangia mwanzo wa mwaka huu kuhusu masuala mbalimbali ambayo ni pamoja na elimu na usalama.
Afisa mkuu wa uchukuzi na barabara katika kaunti ya Kilifi Philip Charo ni kati ya viongozi waliohudhuria kikao hicho katika kijiji cha kiraho.
Wakaazi wa eneo hilo wameeleza furaha yao baada ya ahadi ya taa hilo kufanikiwa kukarabatiwa.

