Mashabiki wa soka la kaunti ya Kilifi wanaiomba klabu ya Bandari Fc kuleta mechi zake za ligi katika kaunti hiyo.
Kwa muendelezo wa Bandari kwenda Kwale kwa mechi zao za nyumbani ni jambo ambalo linawapa mashabiki wa Kilifi ‘wivu’ wa angalau kutazama mechi za vijana hao wa pwani.
Klabu ya Bandari kwa sasa haijakuwa ikitumia uwanja wao wa Mbaraki kutokana na ukarabati unaoendelea (hauko mbali kuisha)
Hata hivyo maswali yanazidi kuibuka iwapo Bandari wangecheza mechi zao Kilifi, ni uwanja upi ungetumika
Kulikuwa na mapendekezo ya awali kuhusu ujenzi wa kiwanja cha hadhi Water Ground Kilifi.
Kulingana na taarifa ni kuwa kiwanja hicho ujenzi wake ulifaa kutamatika mwezi Disemba mwaka huu. Kulishuhudiwa mwanzo mzuri wa hatua za mapema kuujenga uwanja huo kwa kujenga kuta kuuzingira. Unakadiriwa iwapo ungetamatika kufikia Disemba, ungeweza kubeba mashabiki takriban elfu kumi.

