ALI MWACHAUNGA ASEMA AMEACHILIA WACHEZAJI MSIMU HUU

Kocha wa klabu ya Young Bulls inayoshiriki katika ligi ya Fkf daraja la kwanza Ali Marumu Mwachaunga anasema jambo ambalo limemfanya kuwa na mwanzo mbovu msimu huu ni kukosa matayarisho ya kutosha kabla msimu kuanza.

Anasema amelazimika kuachilia wachezaji wengi ambao anadhani hawangemsaidia na badala yake amefanya usajili wa wachezaji wapya, vijana ambao anasema matumaini yako wataiweka Young Bulls katika nafasi nzuri

”Nimelazimika kuachana na wachezaji wengi kwa sababu niliona kuna baadhi nilikuwa siwatumii sanasana. Na hii nilifanya baada ya kuwa nimeanza kuona mwanga katika kikosi changu na wachezaji ambao nilipendelea kuwatumia. Hata hivyo saa hii nimefanya usajili wa wachezaji pale katikati ambao watanisaidia zaidi kuimarisha sehemu hiyo” Alisema Mwachagunga

Marumu anasema Kati ya wachezaji aliowasajili ni Marco Cena mchezaji wa zamani wa Malindi Progressive Academy ambaye anahisi ataleta uzoefu katika sehemu ya kiungo