MANDONGA KUREJEA NCHINI KENYA

Bondia wa Kenya Daniel Wanyonyi analenga kulipiza kisasi kwa bondia wa Tanzania Karim Mandonga wawili hao watakapokuwa wanashuka ulingoni tena kwezi Julai tarehe 22 mwaka huu.

Kwa upande wake Mandonga amemuambia Wanyonyi kwamba analenga kuja na ngumi nyingine ya kigeni na kumtandika huku akizidi kujipiga kifua kwamba hakuna bondia wa Kenya anayeweza kumpiga Mandonga kutoka Tanzania.

”Hapa Kenya hakuna bondia hata mmoja anayeweza kunipiga. Hata huyu Wanyonyi nitampiga tena tu. Kwanza saa hii nakuja na ngumi nyingine ya kigenia ambayo yajawahi kuiskia.” Alisema Mandonga wikendi ilopita alipokuwa akihojiwa na wanahabari.

Wanyonyi kwa upande wake anasema ako tayari kurekebisha makosa na kusajili ushindi nyumbani atakapokuwa anachuana na Mandonga.

Katika pigano la awali mapema mwaka huu Mandonga alitamba katika ukumbi wa KICC baada ya kumtandika Wanyonyi.