MANDONGA KUREJEA KENYA KWA PAMBANO JINGINE

Bondia wa Tanzania Karim Mandonga maarufu kama Mtu Kazi ameratibiwa mechi ya marudio na bondia wa kenya Daniel Wanyonyi tarehe 18 mwezi Machi jijini Nairobi.

Mandonga, alikuwa amepangwa kupambana dhidi ya bondia mwengine raia wa Kenya anayeishi Marekani Raymond “King Kong” Ochieng, ila anahitajika kupunguza uzani wa kilo 15 kabla ya pigano hilo, swala linaonekana kuwa vigumu kuafikia chini ya kipindi cha mwezi moja.

Kwa mujibu wa rais wa shirkisho la wanabondia wakulipwa nchini Kenya (KPBC) Reuben Ndolo wamelazimika kupanga pambano lengine la haraka kati ya Mandonga na Wanyonyi.