Uhaba wa ufadhili kwa vilabu vya soka vya mashinani unasalia kuwa saratani hali ambayo imepelekea kupungua kwa washiriki wa ligi ya eneo bunge la malindi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na mkufunzi wa kathama fc Kalume Kahindi ni kwamba shirikisho la soka la fkf kwenye msimu mpya utakaoanza rasmi wikendi ijayo kumesajiliwa vilabu 18 pekee na sasa ligi itakuwa ya eneo moja tofauti na msimu uliopita uliokuwa na maeneo mawili.
Mkufunzi huyo ametoa wito kwa viongozi wa bunge la kaunti ya kilifi kupitisha miswada ambayo itawezesha kupatikana kwa mgao wa fedha za michezo zitakazosaidia shuhuli za ligi kuendeshwa kwa ubora zaidi.

