Mkurugenzi wa elimu kanda ya pwani Luka Kangogo amesema kaunti ya Kwale ni miongoni mwa kaunti za pwani ambazo hazijaafikia asilimia 100 ya watoto ambao wanapaswa kujiunga na kidato cha kwanza na wale wa Sekondari msingi.
Akizungumza katika kaunti ya Kwale Kangogo amesema wazara ya elimu imeanzisha harakati za kuhakikisha wanafunzi wote katika viwango hivyo wanajiunga na madarasa hayo.
Amesema ni wanafunzi elfu 8 ambao bado hawajajiunga na kidato cha kwanza katika kaunti ya Kwale.
Kwa upande wake naibu kamishna wa eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale Lucy Ndembo ameahidi kushirikiana na machifu pamoja na wazee wa nyumba kumi kuhakikisha asilimia 100 inaafikiwa.
Wakati huohuo Dorothy Kamwilu ambaye ni mshauri wa masuala ya ufundi katika wizara ya elimu amesema kampeni ya kuwapeleka watoto shule inalenga kuhakikisha hakuna mwanafunzi ambaye anakosa kuendeleza masomo ili kuiafikia ndoto zao za maisha.
KAUNTI YA KWALE IMESAJILI IDADI NDOGO YA WANAFUNZI AMBAO WANAJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

