Mbunge wa Nyali kaunti ya Mombasa Mohamed Ali amesema wataendeleza harakati za kuharamisha suala la mapenzi ya jinsia moja bungeni.
Amesema tabia hizo zinakiuka maadili ya kidini pamoja na mila za kiafrika ambazo zinasukumwa na mataifa ya kigeni ili kuendelezwa nchini Kenya.
Ali ambaye alikuwa akiwahutubia wenyeji wa eneo bunge lake la Nyali amesema ni lazima hilo likomeshwe na hawaturuhusu uovu huo kuendelea katika taifa hili.
Mohamed Ali amesema kuna baadhi ya mashirika ambayo sio ya kiserikali na yanafadhiliwa na mataifa ya nje ambayo lengo kuu ni kuhakikisha mapenzi ya jinsia moja yanafanikishwa nchini.
Amewataka Wakenya kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda watoto dhidi ya Ushoga na Usagaji katika taifa la Kenya.
Vilevile, amesema hakuna dini ambayo inaunga mkono mapenzi ya jinsia moja na kuwataka wananchi kuzingatia mafunzo ya dini.
MOHAMED ALI ASEMA WATAENDELEZA MIKAKATI YA KUHARAMISHA SUALA LA MAPENZI YA JINSIA MOJA BUNGENI

