Shirika la kijamii la Faza Youth Action Group kaunti ya Lamu limeitaka serikali ya kaunti hiyo kuharakisha mchakato wa kuzifufua na kuziimarisha zahanati ambazo ziko katika wadi ya Basuba eneo la Boni ili kuwanufaisha wenyeji wa maeneo hayo.
Kulingana na shirika hilo, wadi ya Basuba iko na zahanati moja pekee eneo la Kiangwe na haina uwezo wa kuwahudumia wenyeji wote wa eneo hilo.
Aidha, shirika hilo limesema wenyeji kutoka vijiji mbalimbali katika eneo hilo wamekuwa wakilazimika kutembea mwendo mrefu ili kupata huduma za matibabu hali ambayo imekuwa ikiwahangaisha zaidi.
FAZA YOUTH ACTION GROUP YAITAKA SERIKALI YA KAUNTI YA LAMU KUZIFUFUA NA KUZIIMARISHA ZAHANATI

