MANCHESTER UNITED YASIMAMISHWA NA LEEDS

Klabu ya Manchester United katika ligi kuu nchini Uingereza imekabwa sare ya mabao 2-2 walipokuwa wanashuka dimbani dhidi ya Leeds United katika uwanja wa Old Trafford.

Wilfried Gnonto raia wa italia mwenye umri wa miaka 19 aliipa uongozi Leeds  katika dakika ya kwanza ya mchezo kabla ya Rafael Varane kuiponza the Red Devils kwa kujifunga bao katika dakika ya 48 ya mchezo.

United walilazimika kutoka nyuma na kulipiza mabao hayo kupitia Marcus Rashford pamoja na Jadon Sancho.

Kwa matokeo hayo sasa Manchester united inasalia katika nafasi ya tatu na alama 43 wakati Leeds United ikisimama katika nafasi ya 16 wakiwa na alama 19.