BENSON OMALA YWAZIDI KUONYESHA UBABE

Benson Omala, fowadi wa klabu ya Gor Mahia anazidi kuonyesha ubabe wake katika ligi kuu ya FKF kwa kuzidi kuchana nyavu za upinzani.

Bao lake la jana dhidi ya wanamvinyo Tusker FC linafikisha idadi yake ya mabao hadi 12 baada ya mechi 13 za ligi kuu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Western Stima amekuwa kiungo muhimu katika ushindi wa mechi za Gor Mahia msimu huu na mkufunzi wake Johnnathan McKinstry ambaye awali alimtaja kama mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kushinda kiatu cha dhahabu msimu huu kulingana na kiwango kizuri alicho nacho kwa sasa.