MAN U YAPONGEZWA KWA ZIRO

Wakenya wanazidi kupongeza usajili wa Emmanuel Ziro katika kikosi cha wachezaji wachanga katika klabu ya Manchester United.

Hii ni baada ya mwandishi wa soka maarufu duniani Fabrizio Romano kupachika Picha ya Ziro kwenye ukurasa wake wa Facebook

Wakenya wamemiminika kwenye sehemu ya kutoa maoni ya ukurasa huo wakijivunia kinda huyo kwenye umri wa miaka 16

Taarifa zasema kuwa klabu ya Liverpool na Arsenal zilitaka kumsajili kabla ya maskauti kufikia makubaliano na Manchester United

Taarifa hizo zimepongezwa na wapwani wengi kwa siku kadhaa wiki hii baada ya kubainika kuwa Ziro ni mzawa wa pwani baadhi ya taarifa zikisema anamizizi yake katika mitaa ya Tezo