Pep Guardiola amesisitiza kwamba hatachukua kazi nyingine ya klabu baada ya kumaliza muda wake kama meneja wa Manchester City, lakini yuko wazi kwa uwezekano wa kufundisha timu ya taifa.
Kulikuwa na uvumi kwamba angeondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa mwaka lakini akaongeza muda wake wa kukaa Etihad kwa mwaka mwingine mwezi uliopita.
Na sasa haitarajiwi kwamba ataongeza mkataba tena.
Guardiola hapo awali alionyesha nia ya kufundisha katika ngazi ya kimataifa baadaye katika taaluma yake, na wakati fulani alihusishwa na kazi ya timu ya taifa ya Brazil.
Msimu huu kocha huyo amekuwa na kipindi kigumu katika dimba la Etihad baada ya majeruhi kuathiri kikosi chake kwa ukubwa. Kwa sasa Man City imelemewa kuandikisha matokeo bora sio ligi kuu pekee bali hata kwenye michuano ya UEFA.

