Kocha mpya wa Liverpool Arne Slot ambaye ameanza kibaruachake kwa kasi ya kuridhisha kwa mabosi wake pamoja na mashabiki anasema kuwa analenga kujirekebisha kwenye kupeana maelekezo wakati mechi ikiendelea anapowarekebisha wachezaji wake katika mbavu za uwanja wanaposimama wakufunzi.
Amedokeza kuwa baadhi ya marefa sasa wameanza kukosa kumwelewa jinsi anavyofoka na kuhisi kuwa huenda anakosa nidhamu jambo ambalo limemfanya kuwa kati ya makocha wanakula kadi za njano mara kwa mara uwanjani msimu huu
Kwa mfano leo, kutokana na kadi za njano alizopata awali kocha huyo wa Liverpool anatarajiwa kutumikia adhabu ya kadi hizo kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Southhapton usiku wa leo.
Wikendi Arne Slot alikula kadi ya njano ambayo ilikuwa ya tatu katika mechi ya ligi kuu uingereza walipokuwa wanacuana na Fulham FC Jumamosi. Kocha huyo pia alionyeshwa kadi ya njano dhidi ya Chelsea na Arsenal

