ENGIN FIRAT AJIUZULU

Kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat amejiuzulu hii leo kufuatia majuma kadhaa yaliyopita kushindwa kuipeleka timu hiyo ya taifa kwenye michuano ya AFCON 2024.

Firat amechukua maamuzi hayo baada ya matokeo duni kwenye mechi za kutafuta tikiti ya kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Morocco

Hata hivyo kabla ya kujiuzulu kwake kulikuwepo na tetesi kuwa huenda angefutwa na uongozi mpya wa Shirikisho kutokana na shinikizo la mashabiki waliokuwa wanadai kocha huyo amefeli wakenya

Muda mchache baada ya Firat kujiuzulu rais mpya wa FKF Hussein Mohamed amedokeza kuwa huenda mchakato wa kutafuta kocha mpya ukaanza mara moja huku akisusa kuweka wazi iwapo kocha huyo atakuwa mkenya au kutoka taifa la kigeni