Timu ya taifa ya mpira wa wavu Malkia strikers ambao wako nchini Serbia kwa sasa wanaposubiri kuekea nchini Uholanzi kwa mashindano ya kombe la dunia, wamepoteza mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Serbia Red Stars kwa seti tatu bila jawabu.
Kenya imeratibiwa kuvaana na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye mechi ya kufungua mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 23 mwezi October mashindano yatakayofanyika katika taifa la Uholanzi lakini pia Poland.
Malkia Strikers inayoongozwa na mkufunzi Paul Bitok imekuwepo nchini Brazil kwa kambi ya miezi miwili na nusu wanapojitayarisha kwa mashindano hayo, huku mkufunzi Bitok akiwa na imani kuwa mazoezi hayo yamewaimarisha kungangania ubingwa msimu huu.

