Mkufunzi wa klabu ya Kenya Police Pamzo Omollo amesema kwamba anaimani vijana wake watafanya vyema katika msimu mpya wa mwaka 2022/2023.
Hii ni baada ya kuwa na kipindi kizuri cha maandalizi ya msimu kwani mpaka kufikia sasa wameshinda mechi sita kati ya saba za kirafiki mbali na kupoteza mechi moja dhidi ya Bidco United wikendi iliyopita walipotandikwa kichapo cha mabao 3-2.
Mkufunzi Omolo amesema kuwa kuwepo na mkanganyiko wa iwapo msimu utaanza lini kunazidi kuvunja morale wa wachezaji pamoja na wakuu wa vilabu ambao wanatumia hela ndefu kujiandaa kwa mechi.
Ameomba uongozi wa soka la Kenya kutangaza rasmi tarehe ambayo msimu mpya utaanza rasmi ili kuupa mchezo huo mwelekeo.

