MAAFISA WA POLISI TAITA TAVETA WAANZA KUPEWA USHAURI NASAHA

Maafisa wa polisi kaunti ya Taita Taveta wameanzishiwa zoezi la kupewa ushauri nasaha kutokana na visa vya msongo wa mawazo vinavyosababisha baadhi yao kujitoa uhai.

Idara ya usalama kaunti hiyo kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hiyo ya Taita Taveta wanaendeleza mpango huo wa kuwashuri maafisa wa usalama.

Kulingana na afisa mkuu wa polisi eneo bunge la Taveta Ibrahim Muchuma msongo wa mawazo mara nyingi ndio husababisha maafisa wa usalama kujitoa uhai mbali na changamoto nyinginezo zinazowakumba wakiwa kazini.

Muchuma pia amewashauri wananchi kushirikiana na maafisa wa polisi kwa minajili ya kukabiliana na utovu wa usalama katika jamii.