LALAMA ZAIBULIWA KAUNTI YA KWALE KUHUSU UTEUZI WA WAWAKILISHI WA WADI

Baadhi ya wanachama wa PAA, UDA na ODM kaunti ya Kwale wanalalamikia uteuzi wa wawakilishi wa wadi katika bunge la kaunti hiyo wakisema nafasi hizo za uteuzi zimetolewa pasi na kuzingatia uwakilishi wa watu wenye uwezo maalum na wale wanaotoka katika jamiii ndogo.

Wanachama wa ODM, wamesisitiza kuwa nafasi za uteuzi zilipeanwa kwa watu ambao sio wapiga kura katika kaunti ya Kwale huku wale wanachama wenye uatilifu wakieleza kugadhabishwa na hatua ya usimamizi wa vyama sambamba na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa kutowapa nafasi yoyote.

Aidha wametishia kujitoa kwenye chama hicho iwapo hawatapewa mwafaka wa kina kuhusu utata huo kwa sasa.

Kwa upande wao watu wenye uatilifu kaunti hiyo ya Kwale wametaka uteuzi huo kufanywa upya kwani haukujumuisha watu wenye uwezo maalum kaunti hiyo licha ya kuwa ni haki yao kupata uwakilishi katika bunge la kaunti.