Vijana wa Tana delta kaunti ya Tana River wametakiwa kujiepusha na ngono za kiholela ili kuepuka kuambukizana magonjwa ya zinaa.
Daktari anayesimamia kitengo cha maradhi ya kuambukizwa kaunti ndogo ya Tana delta Daniel Mabombe amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezeka kutokana na idadi kubwa ya vijana kushiriki ngono za kiholela.
Mabombe amesema takwimu zinaonyesha kuwa utumizi wa mipira ya kondomu umepungua kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo jambo linalochangia ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mabombe amesema ni sharti wakaazi wa eneo hilo wajitokeze ili wapimwe wajue hali zao za kiafya mbali na shinikizo za kuwataka kujikinga kupitia mipira ya kondomu sawia na kuepuka ngono za kiholela kama mbinu ya kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

