LOOKMAN AZUNGUMZIA FURAHA YA BALLON DOR 2024

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Ademola Lookman ameeleza kufurahishwa kwake na kutajwa kwenye orodha ya mwisho ya wanariadha 30 watakaowania tuzo la Ballon Dor mwaka huu

Lookman ndiye mwafrika pekee katika orodha hiyo mwaka huu na raia wa Nigeria wa nane kuwahi kuingia katika orodha hiyo.

Lookman amekuwa na mafanikio makubwa msimu uliopita kwa kuwa aliisaidia klabu yake ya Atalanta kushinda Kombe la Europa, Kombe la kwanza kubwa la Ulaya klabu hiyo imewahi kushinda ndani ya kipindi cha miaka 60.

Anakumbukwa kwa kupiga Hatrick katika fainali ya Europa msimu uliopita dhidi ya klabu moto Bayer Leverkusen ambayo ilikuwa inaongozwa na kocha Xabi Alonso.