Dickson Ndiema, mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwana Olimpiki wa Uganda Rebecca Cheptegei, na kusababisha kifo chake, amefariki kutokana na majeraha ya moto pia katika hospitali ya Eldoret.
Ndiema wiki moja ilopita alimwagia mafuta ya petrol Cheptegei na kumwasha moto jambo ambalo lilimfanya kufariki dunia masaa machache badae kutokana na Mwanariadha huyo wa kike kuungua asilimia 80% ya viungo vyake.
Sababu ya kuchomwa kwa Cheptegei ni mgogoro wa nyumbani kuhusu Mali ambazo pia mwanariadha huyo alikuwa amejinunulia ikiwemo kiwanja.
Tukio la kumuua mwanariadha huyo limekashifiwa na ulimwengu mzima wa riadha baada ya kugonga vichwa vya habari kwa takriban wiki nzima

