POTCHETINO APATA KAZI MAREKANI

Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspers na Chelsea Mauricio Potchettino ni rasmi sasa ndiye mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya marekani baada ya kukubali mkataba na shirikisho la soka la taifa hilo.

Potchettino anachukua mikoba ya mkufunzi Gregg Berhalter aliyefutwa kazi kutokana na kuandikisha matokeo duni yaoiyopelekea USA kuandikisha historia ya kuwa taifa la kwanza kuwa wenyeji wa Copa America kuwahi kutolewa katika hatua za makundi

Potchetinno ambaye ni mara yake ya kwanza kuwa kocha wa timu ya taifa amesema analenga kujenga kikosi kitakachokuwa na ushindani mkubwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2026

Mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yataandaliwa na mataifa matatu ambayo ni pamoja na Marekani, Canada pamoja na Mexico