Hii imekua mara ya kwanza kwa Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool, kubanduliwa Nje ya michuano ya Ulaya baada ya Kushinda mechi ya Mkondo wa kwanza Nyumbani, The Reds wakiiyaga Mashindano ya Klabu Bingwa ulaya hapo jana.
Liverpool walaipoteza kupitia Mikwaju minne kwa Moja ya Penalti, baada ya Kutoka sare ya Goli Moja kwa Ujumla Kufuatia Goli la Osumane Dembele dakika ya Kumi na Mbili ya Mechi, Huku Kipa Gianluigi Donnarumma Akizitema penalty za Darwin Nunez na Curtis Jones.
Benfica, Feyenoord Leverkusen Pia waliyaaga Mashindano wakicharazwa kwa Ujumla Magoli manne kwa Moja, na Matano Sufuri dhidi ya Barcelona, Intermilan na Bayern Munich Mtawalia.
Hili ni shindano la Pili Liverpool ya kocha Arne Slot yatolewa msimu huu baada ya kuyaaga mashindano ya FA majuma kadhaa yaliyopita. Kwa sasa Wekundu hao wa Mersyside wamebaki na fainali ya kombe la Carabao na ligi kuu nchini Uingereza.