AISHA JUMWA AITAKA SERIKALI YA RAILA NA RUTO KUWAHUSISHA WANAWAKE KATIKA MIKAKATI YAO.

Mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini Aisha Jumwa, amemtaka Rais William Ruto kuwateua wanawake kwenye nafasi mbali mbali za uongozi, baada yake kuungana na aliyekuwa mpinzani wake Raila Odinga.

Kulingana Aisha, kama kiongozi katika chama cha UDA, anaunga mkono kiukamilifu hatua yao kuja pamoja, ila kuna haja yao kuhakikisha kuwa wanahusisha viongozi wakike katika maamuzi yao.

Jumwa vile vile amesisitiza haja ya kuharakishwa kwa mchakato wa uteuzi wa waziri wa jinsia katika baraza la mawaziri kitaifa, kwani nafasi hiyo imeendelea kusalia wazi, tangia alipo banduliwa baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z.

Kwa upande wake kiongozi wa maendeleo ya wanawake kaunti ya Kilifi Witness Tsuma, amesisitiza haki na usawa katika ugavi wa nafasi za uongozi, baada ya Raila kuungana na Rais William Ruto.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *