DIMBA PATRIOTES YAJITOA KWENYE LIGI YA FKF

Klabu Ya Dimba Patriots imetangaza rasmi Kujiondoa kwenye Shughuli zozote zinazohusiana na Soka, wakidokeza Changamoto wanazopitia Mikononi mwa Shirikisho la Soka Hapa Nchini, wachezaji wa Timu hio wakiwa huru Kujiunga na Klabu Yoyote ile.

Taarifa Hii Inakuja mwezi mmoja tu baada ya Upande huo wenye Makazi Yake Mjini Nairobi, kubanduliwa Nje ya Michuano ya Ligi NSL, hii ni baada ya mahakama kuu Kutupilia Mbali Kesi yao ya awali ya Kutimuliwa Nje ya Ligi.

Oktoba Mwaka Jana Dimba Patriots walipewa Amri ya kusitisha Maamuzi ya FKF, Ya Kuwabandua nje na Kuwarudisha Mwatate United, Huku kupitia taarifa kwenye mtandao wa Kijamii Klabu Hio ikielezea Kutoridhishwa kwao na Shirikisho la Soka.

Beki wa Arsenal na Wa Timu ya Taifa ya Ufaransa William Saliba, amesema ya Kwamba anataka Kusalia Ugani Emirates ili kushinda Mataji na Upande Huo, Mkataba wake wa Sasa Ukitamatika Mwaka wa Elfu Mbili ishirini na saba.

Kufikia sasa Bado hakujakua na Mazungumzo yoyote kati ya Pande Hizo Mbili, Real Madrid wakijitokeza mstari wa Mbele Kuinasa Sajili wa Beki huyo mwenye Umri wa miaka ishirini na Mitatu.

Mfaransa huyo amezicheza Mechi Mia Moja ishirini na moja na The Gunners, akitengeza ushirikiano mzuri na Gabriel Kwenye nafasi ya beki wa kati, Arsenal Ikiorodheshwa kama klabu yenye rekodi nzuri kwenye Safu ya Ulinzi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *