WIZARA YA ELIMU YAWEKA JITIHADA ZA KUBORESHA MIUNDO MSINGI YA ELIMU NCHINI.

Wizara ya Elimu itajenga maabara 1,600 kote nchini, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wa gredi ya 10, wanasomea taaluma wanazo hitaji kwa mujibu wa muongozo wa mtaala wa CBC mwaka 2026.

Kulingana na katibu kwenye wizara ya elimu nchini Bellio Kipsang, hatua hiyo itasaidia katika kuhakikisha kuwa, kila mwanafunzi anapata fursa ya kusomea taaluma za masuala ya sayansi.

Kipsang, ambaye alikuwa katika kaunti ya Mombasa, amesema kuwa tayari serikali imewekeza katika kuajiri walimu wa sayansi na hata maabara katika idadi kubwa ya taasisi za elimu ya juu, kwenye mtaala wa CBC yaani Senior School.

Aidha, muungano wa walimu wa KUPPET kaunti ya Mombasa, ukiongozwa na katibu mkuu kaunti hiyo Lynette Kamadi, umepinga suala hilo ukisema kuwa utatatiza shughuli za masomo, kutokana na kiasi kidogo cha mgao wa fedha za matumizi, zinazo tumwa kwenye shule hizo ikilinganishwa na majukumu yaliyoko.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *