RAILA ODINGA ASEMA ALISHIKIZWA KUUNGANA NA RAIS WILLIAM RUTO.

Aliyekuwa waziri mkuu katika taifa hili Raila Odinga, amesema kuwa sio yeye aliyeshinikiza kuungana na serikali, ila Rais William Ruto, ndiye aliyependekeza waungane.

Odinga ambaye alikabiliwa na pingamizi kali, katika kaunti ya Kisii mnamo siku ya jumamosi, alipokuwa akitaka kuhutubia umma, ametetea uhusiano wake na Rais Ruto, akisema kuwa bado msimamo wake ni ule wa kutetea haki za wakenya.

Aidha, Raila amesema kuwa hatua yake ya kuungana na kiongozi wa taifa, haina uhusiano wowote na uchuguzi mkuu wa mwaka 2027.

Aidha, ameelezea kuwepo kwa urahisi wa kutetea na kutatua changamoto za wakenya, akiwa ndani ya serikali, kinyume na akiwa katika mrengo wa upinzani.