MKENYA ALIYE ANZISHA KITUO CHA POLISI APINGA MADAI YA KUKAMATWA NA MAAFISA WA USALAMA.

Collins Chepkulei, Mwanaume aliye anzisha kituo maafisa wa polisi kushika doria katika eneo la Cherus kaunti ya Uasin Gishu, amekanusha madai ya kukamatwa na maafisa wa polisi.

Collins amewaonya waandishi wa habari, dhidi ya kueneza taarifa kuhusiana na kukamatwa kwake, jambo ambalo anasema sio la kweli.

Mkenya huyo anayedai kuwa na mwenye umri wa miaka 26, amesema amekuwa akishirikiana na wanajamii katika eneo hilo katika kuanzisha kituo, kutokana na ongezeko la idadi ya visa vya uhalifu katika eneo hilo.

Collins ambaye ni mfanyabiashara, ameelezea kutokuwa na makosa yeyote katika kuanzisha kituo hicho, kwani licha ya wananchi kusisitiza serikali kuanzisha kituo cha polisi, juhudi zao hazijakuwa zikitiliwa maanani huku akiahidi kuendelea kulipa kodi ya kituo hicho, hadi pale serikali itakapo chukua hatua ya kujenga kituo rasmi cha polisi.