MARUFUKU YA POGBA YAISHA

Kiungo wa timu yua taifa ya Ufaransa Paul Labile Pogba ni rasmi sasa marufuku yake ya soka imetamatika leo na anaweza kucheza soka la kulipwa ulaya kama alivyokuwa awali kabla ya kupatikana na makosa ya kutumia dawa za kututumua misuli.

Pogba ambaye amekuwa akipiga tizi katika viunga vya Miami nchini Marekani sasa ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na klabu yoyote itakayohitaji huduma zake.

Awali alikuwa anatajwa kuwa huenda akeelekea katika klabu ya MANCHESTER United lakini kwa sasa hilo linasalia tetesi.

Mechi ya mwisho pogba mwenye umri wa miaka 31 kushiriki katika soka la ushindani ni tarehe 27 mwezi November mwka jana ambako mechi hiyo ya klabu bingwa ulaya iliisha kwa sare tasa, wakati huo alikuwa anaitumikia klabu ya Juventus kule Italia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *