MATANOMANE YOUTH YAZIDI KUJIPANGA

Klabu ya Matano Mane Youth inayoongozwa na kocha Emmanuel Mwalugo inazidisha kujiimarisha zaidi katika kikosi chao kuelekea kutamatika kwa msimu huu kipindi hiki cha usajili wakizidi kuleta wachezaji kambini mwao.

Baada ya kufanikiwa kuvamia kambi ya Malindi UNITED na kuzinasa saini za Julius Menza na James Mwambegu maarufu kama Lukaku sasaklabu hiyo imeonyesha nia ya kutaka kumsaini Cyril Ngari fowadi wa klabu ya Kamtonga FC klabu inayoshiriki ligi ya daraja la pili kutoka kaunti ya Taita Taveta.

MatanoMane Youth kutoka Ganze kwa sasa inasimama katika nafasi ya 6 wakiwa na alama 21baada ya mechi 16.

Huu ndio msimu wake wa kwanza klabu ya Matano Mane Youth inashiriki katika ligi ya kitaifa ya daraja la pili baada ya klabu hiyo kuwa na mafanikio makubwa msimu uliopita.