Klabu ya Leicester City sasa imefufuka kunako Ligi Kuu nchini uingereza kufuatia kuifunga bao 4-0 timu mpya kwenye Ligi msimu huu Nottingham Forest mchezo wa Ligi uliochezwa dimba la King Power.
Leicester City ambayo inanolewa na kocha Brendan Rodgers ilikuwa inavuta mkia kwenye msimamo wa Ligi kuu ambapo sasa ushindi ambao wameupata katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo umeifanya kuondoka huko ikiwa ni afueni kwa kocha Rodgers aliyekuwa na wasiwasi kuhusu kandarasi yake na mabosi wa klabu hiyo.
Mabao ya Leicester yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza James Maddison akifunga mabao mawili, Patson Daka akifunga moja lakini pia Harvey Barnes akiingia kambani mara moja.

