GOR MAHIA HAIKO FREEMASON RACHIER ANAJISEMEA MWENYEWE – SAM OCHOLA

Kamati kuu ya klabu ya Gor Mahia imetoa taarifa kwamba klabu hiyo haijihusishi na masuala ya Freemason kuanzia wachezaji na vitengo vyote vya Kogalo.
Hii ni kulingana na katibu mkuu wa klabu hiyo Sam Ocholla ambaye amehoji kuwa suala la mwenye kiti Ambrose Rachier kusema kwamba yeye ni mmoja wa wa mafreemason ni jambo lake binafsi na wala halihusiani kivyovyote na klabu.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini mwenyekiti wa klabu ya Gor Ambrose Rachier alikiri kwamba yeye ni mwanachama wa freemason tangu mwaka 1994.

Amekuwepo katika klabu ya kogalo tangia mwaka wa 2009 akichukua nafasi ya mwenye kiti Erustus Okul kabla ya kuchaguliwa tena bila kupingwa mwaka 2020 kwa muhula utakaotamatika mwaka 2024.